SALLY WISDOM AWATEKA WA SAUZ AFRIKA... KUPIGA NAO KOLABO...



Na Eric Mutinda -  Gospel Magazine -Kenya
Mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye makazi yake ni nchini Kenya, Sally Wisdom amefanya mazungumzo na Mtandao huu wa Gospel Magazine na kuizungumzia ziara yake ya huko Afrika ya Kusini.
Akizungumza na Gospel Magazine ya Tanzania, Wisdom alesema kuwa safari yake nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kihuduma, yaani kulitangaza neno la Mungu lakini Pia kuitanua huduma yake ya uimbaji ifahamike kimataifa zaidi.

Wisdom ameseama kuwa amepata mapokezi makubwa na ameshangaa kuona kuwa watu wa huko wameukubali mziki wake ambao ni wa kiswahili kitu ambacho kimepelekea aanze kuhudumu mji baada ya mji, lakini pia wengi wanamtaka afanye nyimbo zingine akiwa huko afrika ya kusini kwa kushirikiana na waimbaji wa huko, kitu ambacho mwenyewe ameona ni kizuri na ambacho kitasaidia uimbaji wake kusambaa zaidi  kwa kupata mialiko ya kimataifa zaidi.



Wisdom anatamba na kibao kiitwacho UMETENDA ambapo alishirikiana na mwimbaji mkongwe Annastacia Mukabwa, kibao ambacho kimependwa sana na watu wengi.
akizungumza na Gospel Magazine Wisdom amesema kuwa alikutana na Annastacia katika tamasha na hapo ndipo urafiki wao ulipoanzia.
"... lakini siku moja nilijaribu kumsikilizisha moja ya aidia nilizonazo, ndipo alipopenda sana aidia ya wimbo Umetenda namoja kwa moja akawa tayari kufanya kolabo na mimi..." alisema Wisdom
Akimzungumzia Annastacia wisdom amesema kuwa kwake yeye anamchukulia kama rollmodel lakini pia ni mama yake wa kiroho kwani amekuwa akimuelekeza mambo mengi.

wisdom alipoulizwa ni waimbaji gani anaovutiwa nao, hakuacha kumtaja tena Annstacia, lakini pia alisema ni wengi japo hawezi kuwataja wengi akamtaja Solly, Sinachi na Marehemu Anjela Chibalonza. wote wakiwa ni waimbaji kutoka Kenya.


Wasdom alemalizia kusema kuwa yeye ni Ambassada wa Mungu (Balozi) na katika huduma zake kwa nza yeye ni kiongozi wa Praise, ni mtunzi wa Nyimbo na muimbaji lakini mbali na fani hiyo ya uimbaji, ni Mwanamitindo wa mavazi na Nywele.

Comments