Mwimbaji wa Nyimbo za injili nchini Kenya Alice Lisa, amefunguka na kusema kuwa muziki ni maisha yake kwani ndio wito na huduma yake katika kumtumikia Mungu.
Akizungumza na Gospel 1 Magazine kupitia Mwandishi wetu Eric Kiprotich Mutinda, alise alisema kuwa huu ni mwaka wa nne toka agunduwe kuwa wito wake ni uimbaji kwani alianza rasmi huduma hii miaka mitatu iliyopita.
Alice amesema kuwa yeye ameokoka na anapeda sana kumuimbia Mungu kwani uimbaji ndio wito wake kutoka kwa Mungu baada Mungu kumponya toka katika ugonjwa aliokuwa akiumwa na kurejeshwa katika afya yake kamili.
alifunguka pia na kusema kuwa, Uimbaji wa nyimbo za injli unahitaji Uvumilivu.
"... Nimejifunza kuwa Kila kitu kinachog'aacho huwa hakiji kwa siku moja,.. hivyo muziki huu ni safari ndefu inayohitaji uvumilivu bidii na kujitoa zaidi..." alisema Alice Lisa
Aliendelea kusema kuwa kinachompamotisha kuendelea na uimbaji wakati muziki huu bado haukizi mahitaji yake alikuwa na haya ya kusema.
"... It's a passion, sijui naeza semaje kwa kiswahili (shauku), lakini pili naichukulia kama huduma yangu ya kuwaleta watu kumfahamu Mungu aliye hai na anaye jibu maombi, lakini pia nafahamu kuwa kumtumikia Mungu sio hasara, hela zitakuja tu chamsingi ni kutimiza wito..." alisema Alice.
Alice alisema kuwa muziki huu una changamoto kubwa kwani hakuna barabara ikosayo kona au milima, amesema kuwa mziki huu unahitaji pesa ilikufikia uendako.
Alice alisema kuwa ana nyimbo sita kwa sasa ambazo ni, alikutana nami, Urejesho, Nikiwa Nawe, Mtegemee Mungu, na wimbo mpya ambao ndio anatarajia kufanyia video unaitwa Nina imani Kwako.
akaongeza kuwa anavutiwa na waimbaji kama Christina Shusho wa Tanzania na Sinach kimataifa. akaendelea kusema kuwa ana mipango mingi ya kufanya kuhusiana na muziki wake ila Mengi hawezi kuyasema kwani anaomba uzima, afya na Hekima tu, Mengi mazuri yatafuata.
"... Muziki ni Maisha yangu, Ilove Music, irespect music and ilive in music..." alimalizia Alice
HII HAPA NI VIDEO YA ALICE LISA - UREJESHO
Comments
Post a Comment