MALI ZA LUGUMI HAZITAPIGWA MNADA - MCHUNGAJI MASHIMO... SOMA UNABII HUU




Mchungaji wa Mitume, Maaskofu na Manabii, Commando Mashimo, amekaririwa na mtandao wa Gospel 1 Magazine kuwa Saidi Lugumi anaagizwa kutoa sadaka ya shilingi elfu 10 tu kanisani ili mali zake zote zisiuzwe.
Akiongea kwa msisitizo, Mchungaji Mashimo amesema kuwa mali za Lugumi hazitauzwa siku ta tarehe 9 Mwezi wa 9 ambayo ndio siku iliyopangwa kupigwa mnada kwa mali zake kupitia kampuni ya YONO.
Mchungaji Mashimo ameongeza kusema kuwa hilo ni agizo Kutoka kwa Mungu kuwa Mali zake hazitauzwa lakini kuna kitu anatakiwa kukifanya kabla ya tarehe hiyo kufika.
"... mimi nimeagizwa na Mungu na huu ujumbe ninaotoa ni kutoka kwa Mungu aliye mbinguni... kuwa Mali za Lungumi hazitauzwa siku hiyo ya tarehe tisa,.." alisema Mchungaji mashimo
"... ni kweli Lugumi alifanya makosa na Mungu anaweza kuondoa jeuri yake yote lakini kwa vile yeye ni mwenye huruma, amemuagiza Lugumi akatoe sadaka ya Sh. elfu 10 tu katika kanisa lolote na kila kitu kitakuwa sawa..." alisema Mchunhaji Mashimo
"... Nimeona milango ya Lugumi imefunguka, yaani pembe nne za dunia zimefunguka, hivyo anachoagizwa Lugumi ni hicho tu na kila kitu kitakwenda sawa..." alimalizia kusema mchungaji Mashimo.

Mwisho kabisa alisema kuwa swala la Lugumi ni kama la ayubu, maana Ayubu alikuwa na kila kitu lakini Mungu aliamua kumjaribu, hivyo Lugumi naye Mungu aliamua kumuonesha kuwa ndani ya sekunda moja mtu aweza kuwa masiki na ndani ya sekunde hiyohiyo mtu aweza kuwa tajiri sana , hivyo asifanye mchezo.

Mchungaji Mashimo anapatikana kwa namba +255 655 223 799

18 Tena Bwana akanijulisha haya, nami nikayajua; ndipo uliponionyesha matendo yao. Yeremia 11:18

19 Lakini mimi nalikuwa kama mwana-kondoo mpole achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujuwa kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, natuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena.
Yeremia 11:19

Ufunuo 10:10 - 11

Comments