Mwimbaaji anayechupukia katika medani ya nyimbo za injili na ambaye makazi yake ni Dodoma katika Kijiji cha Matumbulu, Eveline Asheri Ijinji, yuko mbioni kukamilisha Albamu yake katika Studio za Eck Production Magomeni Jijini Dar Es Salaam.
Eveline Ijinji amisema kuwa Albamu yake yenye jumla ya nyimbo sita itakuwa tayari hivi karibuni kwani ndio yuka studio anamalizia nyimbo zilizokuwa zimebaki na tayari wako katika hatua nzuri kwani alishamaliza uimbaji. imebaki kazi ya Producer.
"... ukweli ni kwamba nilikuwa sijapata muda wa kumalizia hii albamu, mwanzo nilifanya nyimbo mbili zikawa zimebaki nne, sasa ukizingatia nitokako ni mbali kidogo na huko nakuwa nimebanywa nashughuli zangu za kila siku nikawa sijapata nafasi... lakini sasa ndio nimekuja kumalizia, na uzuri ni kwamba imebaki kazi ya produce tu kumalizia mixing kwani mimi nilishafanya yangu..." aliongea Eveline Ijinji.
Akiongea na Gospel 1 Magazine Eveline aliongeza kuwa Albamu yake itaitwa SHITUKA na hivi karibuni ataachia wimbo huo uliobeba jina la album kwa ajili ya kuanza kutangaza ujio wa albamu hiyo.
amesema kuwa nyimbo zilizomo ndani ya Albamu hiyo ni pamoja na Shituka, Nakushukuru, Rafiki wa kweli, Nichunguze, Usikae Mabali Nami na Tumshangile Bwana.
Eveline Ijinji amesekuwa yuko tayari kwa mialiko mbalimbali na ukitaka kumpata mpigie simu nambari 0676 213948.
Comments
Post a Comment