PAMELA SENYONGA KUANDAA TAMASHA LA SHUKRANI...



Mwaimbaji wa nyimbo za Injili na Mchungaji Pamela Senyonga mwenye makazi yake nchini Uganda, amesema anaandaa Tamasha la kumshukuru Mungu na kuwashukuru mashabiki wake kwani bila wao asingefika hapo alipofikia.

Akiongea na Mwanahabari wetu Eric Kiprotich Mutinda alioko nchini Kenya, Pamela amesema kuwa anaanda tamasha hilo mapema kipindi hiki lakini hatapenda kutaja ni lini kwani bado yuko kwenye maandalizi na yakishakamilika ataweka kila kitu wazi.

Pamela Senyonga ni mwimbaji ambaye ameanza huduma hii kitambo kidogo, na anasema kuwa alipata uzoefu zaidi alipokuwa katika kundi la Alpha Praise kabla ya kuanza Uimbaji binafsi Mwaka 2007 na kuachia albamu yake ya kwanza mwaka 2008.



Pamela ameendelea kueleza kuwa alianza kuimba toka akiwa shule ya msingi lakini kipaji chake kilianza kuonekana toka alipokuwa alipokuwa mdogo kwani ni hakika kuwa alizaliwa na kipaji cha uimbaji.
Pamela amedumu karika uimbaji wa nyimbo za injili kwa kipindi cha miaka tisa sasa, na anasema katika miaka yote hiyo alikuwa akiongozwa na Roho Mtakatifu ndio maaana kadumu na kuendelea kufanya vizuri. ".. Na zaidi ni uvumilivu na Hekima ndio nguzo yangu Kubwa..."

ameendelea kusema kuwa ili kufikia hapo alijishusha na kufanya Collabo ya waimbaji wengine na kisha kusambaza kazi zake vyuoni ikiwa ni pamoja na kufanya juduma hiyo vyuoni pia.
Pamela amesema kuwa yeye ni mtunzi mzuri tu na nyimbo zake huanza kwa kuandika mwenyewe na ndipo kumtafuta producer wa Audio na Video ambaona hufanya sehemu zao Muhimu.



Pamela amesema kuwa mziki wa Injili ndio unazidi kupakua kwa kasi Nchi Uganda, hivyo anawashauri sana waimbaji wa nyimbo za injili nchini Humo na kwingine kuzidisha bidii hasa katika kuandika jumbe nzuri na kuhakikisha wanafanya nyimbo zenye mvuto na sio kuripua tu.

Comments