ROSE MUHANDO AFANANISHWA NA CHID BENZ: WATU WAFUNGUKA - VYOMBO VYA HABARI



Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili nchini au Malkia wa Gospel Rose Muhando amewafanya watu kuchukia hata kuingia kwenye matamasha yake kulingana na kile kinachosemekana ni tabia yake ya utumiaji wa madawa ya kulevya.

Wakiongea kwa wakati tofauti na Kituo cha Eatv watu mbalimbali walisema kuwa hata wakipewa nini hawakotayari kuingia kwenye matamasha ambayo anaandaa Rose Muhando kwani Hakuna kitu cha maana watakachokwenda kukipata zaidi ya kwenda kumuona Teja akiimba jukwaani.



"... unajua Rose tulizoea kumuona ni mtu mwenye utukufu wa Mungu na ni mtu Mwimbaji ambaye alikuwa anambariki kila mtu kwa nyimbo zake, sasa kulingana na haya mabadiliko yake ya sasa, sidhani kaka mimi naweza hata kwenda kwenye maonesho yake kwani hakuna nitakachokwenda kukipata zaidi ya kwenda kumuona Teja akiimba jukwaani..." aliongea Mdau wa Kwanza.

Mwngine naye alidiriki kumfananisha Rose na Chid Bez kwa kusema
"... yaani mimi nikaangalie onyesho la Rose Muhando?.. siwezi kabisa,.. maana hawatofautiani kitu na Chid Benz, sasa ni sawa unaniambia nikaangalie onyesho la Chid Benz, yaani hata ukinipa bajaji ya bure mimi siwezi..." aliongea mdau mwingine ambaye ni mdereva wa Bajaji.

Kumekuwa na tetesi nyingi na ambazo zimekuwa za muda mrefu sana kuwa Mwimbaji huyo mashuhuri wa nyimbo za ijili ameathirika na madawa ya kulevya kitu kinachopelekea muziki wake kushuka. lakini ukizungumza na Rose kuhusu tuhuma hizi anakanusha vikali.
Gospel 1 Magazine tunaahidi kumtafuta Rose kwaajili ya mazungumzo ili tuweze kupata undani na ukweli wa jambo hili ambalo limekuwa gumzo kubwa kwa watu.

Comments