Mwanamuziki na mwimbaji wa Nyimbo za Injili za kizazi kipya Antony Davidson Owega, au Adishutter, ameweka bayana kuhusu safari yake ya kimuziki na changamoto mbalimbali anazozipitia katika safari hiyo ya Uimbaji.
Akizungumza na Mwandishi wa Gospel 1 Magazine aliyeko nchini Kenya Eric Kiprotich Mutinda, Adishutter ameseka kuwa Mwanzo wa safari yake kimuziki ilikuwa mwaka 2014 na alikuwa bado yuko shule, hapo ndipo kipaji chake kilipojionyesha na kukiweza wazi.
ameendelea kusema kuwa amekuwa ni mtunzi mzuri sana kwani anapotunga mara nyingi huzingatia hadhira au watu wanataka nini ndipo na yeye hufanya kile ambacho anaamini kikiwafikia wasikilizaji watakipokea vizuri na kuhakikisha zinabadilisha maisha yao na hasa vijana kama yeye.
Adishutter alielezea kuwa changamoto nyingi anazozipitia kwa sasa ni upatikanaji wa fedha, lakini pia amesema kuwa upatikanani wa mialiko mbalimbali au shows ni shida sana lakini kwa upande wake anaziamini sana kazi zake naye anajiamini pia.
anasema pamoja na changamoto zote, yeye hana majuto wala hajutii lolote kwani anaamini kuwa kazi ya uimbaji anayoifanya ni wito kwake na nikipaji kutoka kwa Mungu.
Adishutter kwa sasa anatamba na ngoma inayokwenda kwa jina la Makofi ambayo inaendelea kufanya vizuri kwenye vituo mbalimbali ikiwemo mitandao mbalimbali ya kijamii.
Amesema kuwa mpaka sasa anazo nyimbo nne na kwa sasa kuna kazi mpya ambayo anaiandaa na Director wake Gylo Painto.
lakini amemalizia kwa kuwashukuru sana mashabiki wake na kusema kuwa hana cha kuwalipa kwani kama sio wao asingeweza kufika hapo alipofikia.
HII HAPA VIDEO YA ADISHUTTER - MAKOFI
Comments
Post a Comment