ALFREDY FUNDA ASIKILIZA KILIO CHA WENGI...SASA KUSUDI LIKO YOU TUBE...



Mwimbaji wa nyimbo za injili nchi Tanzania Alfredy Funda a.k.a Mze wa Kusudi ameachi rasmi video ya wimbo wake wa Kusudi katika mtandao wa you tube.

Akiongea na Gospel 1 Magazine, Alfredy Funda ambaye pia anatamba na kibao cha Acha nimshukuru Mungu ambacho nacho kipo you tube, alisema kuwa ameamua kuachia wimbo huo mapema kutokana na maombi ya watu wengi ambao waliishausikia lakini wakawa wanatamani kuona video yake itakuwaje.

"... nilitamani sana kusubiri mpaka wimbo wangu wa Acha nimshukuru Mungu ukae japo Miezi kadha au hata miaka kadhaa ndipo niachie video ya wimbo wa kusudi, lakini maombi ya mashabiki na wapenzi wa nyimbo za injili hasa wale wanaofuatilia nyimbo zangu yakawa mengi kwamba wanataka video ya Kusudi, nikawa sina budi..." alisema Funda.

Funda ni Mwimbaji mwenye historia nzito katika uimbaji wa nyimbo za injili hasa ukizingatia kuwa alitokea kwenye uimbaji wa nyimbo za Hip Hop.

Hivi karibuni tutakuletea makala yenye historia nzito ya Alfredy Funda, hatua kwa hatua katika Uimbaji mpaka kulibeba Kusudi.

HII HAPA VIDEO YA KUSUDI

Comments