PATRICIA NGONYANI KUNG'ARA 2018



Mwimbaji wa njimbo za Injili anayechipukia na anayekuja juu kwa kasi, Patricia Ngonyani, ameiambia gospel 1 magazine kuwa mwaka huu wa 2018 ndio mwaka wake wa kung'ara katika medani hiyo ya nyimo za injili.

Akiongea na mwandishi wetu Patricia alisema kuwa mwaka jana yaani 2017 alikuwa amekamatwa sana na shughuli za Ofisi ambako anafanyia kazi ndio maana hakuwa serious sana katika kuihangaikia sana albamu yake ambayo iko tayari toka mwaka jana.
Amesema anaamini kuwa wimbo wake aliouachia toka mwaka jana unaendelea kufanya vizuri katika baadhi ya media ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii, ni wimbo huo unaoitwa Niseme Nini unaoendelea kumuweka juu japo hakuwa serious katika kuupambania.

"... unajua Wimbo wa Niseme nini umeniweka katika nafasi nzuri na sasa nimeamua sasa kupambana, na nilishasema kuwa mwaka huu ni wangu na Mungu wangu anajuwa kuwa waka huu wa 2018 ndio mwaka wangu wa kung'ara,.. najuwa waimbaji sasa hivi tuko wengi sana na ili uonekane unatakiwa kwanza uwe na nyimbo nzuri alafu uzihangaikie, sasa mimi nina albamu nzima ambayo imesheheni nyimbo nzuri tupu sasa sioni sababu gani mwaka huu nising'are?.. "aliongea Patricia mbele ya kipaza cha mwanahabari wetu.

Patricia amesema kwa vile Wimbo wake wa Niseme nini Bado uko juu hawezi kuachia mwingine kwa sasa badala yake anajiandaa kufanya video kali sana ya wimbo huo kabla hajamalizia video ya albamu nzima mapema mwaka huu.

HUU HAPA WIMBO WA NISEME NINI?

Comments