k
TEREHE 30 ya mwezi wa June Itakuwa ni siku ambayo Mkoa wa Lindi utaandika historia mpya katika medani ya Uimbaji wa nyimbo za injili .
katika Tarehe hiyo huku Nachingwea Lindi, kutakuwa na uzinduzi mkubwa na wa kihistoria ambao haujawahi kutokea au kufanyika ndani ya miaka mingi sana iliyopita.
Uzinduzi huo wa Albamu ya Mwimbaji Flora Chilumba mwenye Makao yake huko Nachingea na ambao Umeandaliwa na Kanisa la FPCT Nachingwea, utawakutanisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka karibia kila kona ya Tanzania ambao Wote watakwenda kumsindikiza Mwimbaji mwenzao katika uzinduzi huo utakaofanyikia katika Kanisa la EAGT Mashujaa Nachingwea.
Akiongea kwa njia ya simu na Mwandishi wa Gospel 1 Magazine Flora Chilumba alisema kuwa Maandalizi yanaendelea na watu wa Nachingea wanaisubiria tarehe hiyo kwa hamu kubwa.
"... kusema ukweli maandalizi yanaendelea vizuri, na wakazi wa Lindi na Nachingwea wana hamu kweli ya kuona waimbaji kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wakihudumu kwani ni jambo ambalo halijawahi kutokea huku kwetu... yaani hata sijui... maana matangazo tu yalipoanza kuwekwa basi kila mtu anatamani siku hiyo iwahi kufika..." alisema Flora
Waimbaji watakaomsindikiza Flora Chilumba katika Uzinduzi huo wa kihistoria ni pamoja na. Honoratha Muzuli toka Dodoma, Patricia Ngonyani kutoka Tanga, Amani Chimalamugo Kutoka Dar es Salaam, Sarah Mtambo Kutoka Tanga, Mussa Sikabwe Kutoka Dar es Salaam, Kiza Blessing Kutoka Dar es Salaam, Evelina Ijinji Kutoka Dodoma, Faraja Ngomongo Kutoka Lindi, Patricia Mnali Kutoka Lindi, Dino Zenu wa Nachingwea na wengine wengi, na huku Kwaya mbalimbali zikilipamba tukio zima la Uzinduzi.

Comments
Post a Comment