"... Mimi nawaonehuruma sana, Watoto yatima walivyotelekezwa, ni watoto wasio na uwezo,.. nimepita mitaani nimewaona, nimepita majumbani nimewaona wanavyosononeka na kuumia kwa maumivu makali..."
Haya ni maneno ya kwake Glory Massawe, Mwimbaji wa nyimbo za injili anayekuja juu kwa kasi.
amesema maneno hayo yako katika Wimbo wake unaoitwa Yatima ambao pia uko katika Albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Tukaze Mwendo ambayo iko jikoni na ambayo itakuwa mitaani ndani ya siku hizi chache zijazo.
Akiongea na Gospel 1Magazine Glory amesema kuwa, kuimba kwake wimbo huo kulitokana na hisia alizonazo dhidi ya watoto yatima kwani anatamani kama angekuwa na uwezo mkubwa aweze kuwasaidia wote, lakini kwa vile uwezo wake sio mkubwa, ndio maana aliamua kuimba wimbo huo uwe kama wito kwa watu wote wenye mioyo ya huruma waweze kuwasaidia watoto hao wanaohangaika na kuteseka mitaani bila mdaada.
Albamu ya Glory Massawe itakuwa mitaani hivi karibuni kwani video ziko katika hatua ya mwisho kuandaliwa chini ya kampuni ya Studio 21 na Director MO Design.
Comments
Post a Comment