ISAYA OSCA KUWANUFAISHA YATIMA, WAJANE NA WAZEE KATIKA TAMASHA LA UZINDUZI WAKE...

Mwimbaji na Mwinjilisti Isaya Osca



Muimbaji wa Nyimbo za Injili na Muinjilisti Isaya Osca, anatarajia kuzindua albamu yake Iitwayo Bwana Washangaza huko Tanga kwa ajili ya kuwasaidia wasiojiweza na wenye matatizo.


Uzinduzi huo utakaofanyika katika eneo la kwa Gunda Korogwe mjini Tanga siku ya Jumaa pili ya Tarehe 30/09/2008 katika viwanja vya kanisa International Pentecost, utakuwa na lengo kuu la kuwasaidia wasio jiweza kama vile Wajane, Wagane, Yatima, Walemavu na wazee.
Tamasha litaanza saa Saba (7) mchana na kumalizika saa kumi na mbili (12) Jioni kwa kiingilio cha Sh. 3000 Wakubwa na 1000 kwa watoto,

Tamasha hilo litapambwa na waimbaji mbalimbali wa injili kutoka pande mbalimbali, likiongozwa pia na Askofu Petro Kamandwa.


Akiongea na Gospel 1 Magazine Isaya Osca amesema kuwa ameamua kufanya Hivyo kwa sababu tu moyo wake umeguswa kuwa saidia watu hao wasiojiweza, ukizingatia kuwa baadhi ya watu hupenda sana kuwanyanyapaa watu hao wenye matatizo na kushindwa kuwapa msaada.

"... kusema ukweli mimi nimeguswa tu kufanya Huduma hii, kwangu mimi kuwasaidia watu wenye shida ni huduma,.. unajuwa watu hawa wenye matatizo wanapenda sana kutengwa na baadhi ya watu na kuwaona hawafai, lakini pia utakuta kuna watu wana uwezo na wako katika posistion nzuri ya kuweza kuwasaidia watu hawa lakini wanashindwa kufanya hivyo... Alisema Osca

"... mimi kwa hicho kidogo nitakachokipata huko Tanga nitakigawa kwa Yatima, Wajane, Wagane, Walemavu na Wazee, hivyo ndivyo nilivyoongozwa kiufanya... alimalizia


Osca anawaomba watu wa Tanga wajitokeze kwa wingi ili waweze kufanikisha shughuli hiyo iende kama ilivyopangwa na watu hao wenye Matatizo wapate msaada kama alivyoongozwa...

Comments