Mwimbaji wa nyimbo za Injili na anayetamba kwa sasa na kibao cha Baba yetu Sarah Mghamba, anapenda kuwaalika katika uzinduzi wa albamu yake, inayokwenda kwa jina la Baba Yetu.
Akiongea na Mtandao huu Sarah Mgamba Mwenye makazi yake Mkoani Tanga, amesema kuwa Uzinduzi huo utakuwa wa kihistoria sana kwani utahudhuriwa na waimbaji mbalimbali kutoka karibia kila kona ya Tanzania.
Aliendelea kusema kuwa mkutano huo utahudhuriwa na Waimbaji kama Vile Flora Chilumba Kutoka Lindi anayetamba na Wimbo wa Tulingane, Honoratha Mzuli Kutoka Dodoma anayetamba na wimbo wa Tumbo Niache, Patricia Ngonyani toka Tanga anayetamba na wimbo wa Niseme Nini, Sister amani toka Dar es Salaam anayetamba na wimbo wa Pigania Haki yako, Mussa Sikabwe Kutoka Dar es Salaam anayetamba na nyimbo kama Ebeneza na Ndiwe Mfalme.
wengine ni Emmy Charles Kutoka Dar es Salaam, Evelina Ijinji Kutoka Dodoma, Nelly Rebium kutoka Tanga Jesca Godwin Kutoka Tanga, Chris Anney kututoka Tanga na wengine wengi sana.
Aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na waimbaji binafsi, pia kutakuwa na kwaya mbalimbali kama vile kwaya ya Kilindi Cha Baraka T.A.G Songe pamoja na Upendo Kwaya ya Anglikana Songe.
Uzinduzi huo utafanyika siku ya Tarehe 15 /09/ 2018 katika Kanisa la T.A.G Songe Mkoani Tanga kuanzia saa 7 mchana.
Comments
Post a Comment