Mwimbaji wa Nyimbo za injili anayetamba na Kibao kinachokwenda na jina la GUSA MOYO WANGU, Kinachofanya vizuri kunako Medias na Mitandao mingine yakijamii, Glory Massawe, ameachia Ngoma yake mpya inayokwenda kwenda kwa jina la TUSHIKAMANE WATANZANIA.
Ngoma hii ambayo Video yake ilifanywa chini ya Director MO Design, imeingia rasmi leo katika mtandao wa You tube na kusambazwa pia katika media mbalimbali.
Akiongea na Gospel 1 Magazine Glory Massawe alisema kuwa Wimbo huu aliutengeneza rasmi kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli katika juhudi zake za Kuijenga Nchi kwa kufanya Kazi.
"... unajua hata sisi waimbaji wa nyimbo za injili tuna haki ya kumsapoti Raisi wetu kwa Juhudi anazozionesha za makusudi kabisa zakuijenga inchi yetu, ujuwe ni kweli bila kufanya kazi nchi haiwezi kusonga mbele, sasa sisi waimbaji tunatakiwa kumsapoti Raisi wetu angalau kwa kutunga nyimbo zinazohimiza ufanyaji kazi pia... alisema Glory Massawe.
Glory alisema yuko Tayari hata ziara mbalimbali za kuhamasisha Watanzania katika Ufanyaji kazi kama tu atapewa kibali hicho. lakini alikuwa pia anaomba wimbo huu usambazwe kwa nguvu zote ili kuendelea kuhamasisha ufanyaji kazi.
anapatikana kwa namba +255 758 716 186

Comments
Post a Comment