ROLL MODEL WA AKINA CHIBALONZA NA BUKUKU CATHERINE KYAMBIKI AIBUKIA MO DESIGN STUDIOS AKITOKEA KENYA

Mwimbaji Catherine Kyambiki Akiwa na Maproducer Wake

 
 Mwimbaji Nguli wa Wa Nyimbo za Injili na Roll Model wa Waimbaji wengi Tanzania Catherine Kyambiki, Ameingia Tanzania na kuibukia ndani ya studio za MO Design na kukutana na Maproducer wanaozamilia kumfanyia makubwa.

Akitokea Jijini Nairobi Nchini Kenya ambako ndo anakofanyia shughuli zake kwa sasa, Kyambiki ameiambia Gospel 1 Magazine kuwa amekuja rasmi kwajili ya kutengeneza nyimbo Tatu na Video ndani ya Studio hizo za MO Design.
Amesema lengo lilikuwa ni kutengeneza Audio tu, lakini baada ya kukuta kuna huduma nyingi katika Studio hizo, ameamua afanye kila kitu hapo ili arudi Nairobi na kazi zilizokamilika.

"... unajuwa mimi nilijuwa ntafanya Audio tu na kuondoka, lakini baada ya kukuta kumbe wanafanya mpaka video, ku Design ma cover kufanya Promotions, yaani hapa nimefika..." Alisema Kyambiki.

Catherine Kyambiki ni Mwimbaji ambaye ndo aliyewafanya mpaka wakina Anjela Chibalonza kuanza kuimba na kujulikana, Akina Bahati Bukuku walikuwa wakiiga style zake na hivyo kupata njia ya Kutokea.




Comments